Wednesday, July 15, 2020

NANI KAMA HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI?


      JOHN POMBE MAGUFULI aliapishwa kuwa Rais wa tano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 5,2015.hadi kufikia Jul 11.2020 siku ambayo alipigiwa kura za  maoni kuomba nafasi nyingine anatimiza siku 171O
Napo alipita kwa kishindo kwa aslimia 100%
Naomba nikueelezee baathi za kazi alizo zifanya kipindi hicho kifupi
  1. kudumisha amani.usalama na utulivu nchini
  2. kafanikisha serikali kuhamia dodoma
  3. kajenga Reli ya kisasa(SGR)
  4. kajenga viwanda
  5. kanunua ndege
  6. kajenga barabara juu sehemu za Ubungo.Tazara na mataa ya chang’ombe inaendelea kujengwa
  7. kajenga bwawa la umeme rufiji la nyerere
  8. bandari mpya zimeongezwa
  9. sheria za madini zimebadilishwa \
  10. kafanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati
  11. kafanikiwa kurejesha mali za uma
  12. Kaweza kupambana na rushwa na kuwakamata watuhumiwa nakuwafunga jele watuhumiwa
  13. Elimu bila maripo
  14. vituo vya afya na zahanati zimeongezwa
  15. barabara za lami zimejengwa kila sehemu hata kwetu kiwalani tunpita kwenye lami na mataa yanawaka
  16. umeme mpaka vijijini umefika
  17. kuweza kukusanya mapato makubwa ambayo hayajawai kutokea tangu nchi ipate uhuru
  18. kafanikiwa kupunguza wizara
  19. kupunguza uingiaji wa madawa ya kuleevya nchini
  20. kuwaachisha kazi watu wenye vyeti feki
  21. kajenga mashule mengi nchini
  22. kafanikiwa kuzibiti mfumuko wa bei nchini
  23. kilimo kimeongezeka na mavuno yameongezeka mazao ya chakula
  24. kaongeza watumishi wa afya
  25. kafanikiwa kupunguza umasikini nchini
  26. kafanikiwa kusamehe wafungwa
  27. kafanikiwa kujenga mahakama za mafisadi
  28. kafanikiwa kufuta kesi za mahabusu nchini
  29. kafanikisha kutoa vitamburisho vya wamachinga nchini
hizi ni baathi za kazi alizo zifanya aliyekuwa Rais wetu mpendwa hayati DK JOHN POMBE
 MAGUFULI
Baba safari yako ni nyeupe sana kwani watu wamejionea wenyewe watu wanavyo kulilia Uwanja wa vijana unakutakia pumuziko lili jema kwani kazi ya mungu haina makosa

Tuesday, May 12, 2020

KAZI ZA MKATABA.


Uwanja wa vijana unao uwezo wa kufanya kazi za mkataba na mtu kwa mfano, unanunua kitendea kazi chenye thaman ya Tsh. 1000000/= unarudishiwa Tsh. 1500000/= ndani ya Miezi Mitano au sita.

USULUHISHI AU MAPATANISHO.


Uwanja wa vijana unatoa huduma bure kusuluhisha ,migogoro ya aina mbalimbali pia inatoa upatanisho wa aina mbalimbali.

Kwa wana Ndoa uwanja wa vijana unaziboresha ndoa ambazo zimefikia hali ya mahututi bureee.

Kwa wana Ndoa Waliokimbia nyumba zao. uwanja vijana unazo njia za kuwarudisha hata kama haonekani atarudi mwenyewe nyumbani awe Baba Awe Mama

HABARI NJEMA KWA MTU ANAYETAKA KUONGEZA KIPATO KATIKA KIPINDI CHA MTIKISIKO WA UCHUMU DUNIAN.


Uwanja wa vijana unazo njia mbili ambazo mtu anaweza akazitumia kuimarisha uchumi wake katika kipind hiki.

Pia anaweza akabuniwa mradi ambao utaendana na yeye jinsi alivyo kwa mtaji mdogo sana, pia kwa watu wanaotaka kuzalisha mali akiwa kazini pia anaweza kusaidiwa. 

Kwa watu walioachishwa kazi au wameyumba kimaisha pia wanaweza kutengenezewa kitu cha kufanya kuendana na hali yake aliyonayo zingine hata za mtaji kuanzia Tsh. 10000/=.

Monday, March 16, 2020

HABARI NJEMA KWA WATU WANAOTAKA KUANZISHA BIASHARA, MRADI AU KUTAKA KUBUNI, KUBORESHA MRADI AU BIASHARA WATASAIDIWA BURE.

Uwanja wa vijana utakusaidia  bure kwa mambo yafuatayo ili mtu asije akapata hasara  katika biashara yake kabla haijaanzishwa au imeanzishwa tayari baadhi ya mambo yenyewe ni haya yafuatayo;

1. kubuniwa mradi au biashara ambao hautaweza kukupa hasara.

2. Kukutafutia sehemu ya kuweka mradi wako au biashara yako.

3. Kukufanyanyia mchanganuo wa mradi au biashara yako.

4. Kukupa majibu au muelekeo wa biashara yako au mradi wako          kama upo hai au umekufa.

5. Kukufanyia mchanganuo wa mkopo unaohitajika kwenye                biashara yako au mradi wako ili usije ukapata hasara katika              marejesho yako.

6. Kukuelezea mambo ya kuzingatia kuyafanya kabla hujaanzisha        biashara au mradi.

7. Tutakusaidia kurasimisha (kusajili) mradi wako au biashara              yako.

8. Tutakusimamia biashara au mradi wako na tutakupa ushahuri          bure kabisa ndani ya miezi sita ya mwanzo.

9. Tutakusaidia kukutafutia soko la bidhaa zako.

10. Tutakukagulia huduma yako kama inaviwango vinavyohitajika        au haina viwango.

11. Tutakusaidia kukupa mbinu za kushinda kwenye soko la                  ushindani katika eneo unalofanyia biashara au mradi.

Thursday, February 20, 2020

HABARI NJEMA KWA VIJANA WA KITANZANIA

1.Je umewahi kujiuliza kuhusu fursa zinazopatikana Tanzania?

  • Unazitambua fursa zinazo tolewa na serikali kwa vijana?
  • Umejiandaaje na fursa zinazoandaliwa na serikali kwa vijana?



  • Je unaziona hizo fursa? Au hauna jicho la tatu la kuziona fursa hizo?

Au wewe ni miongoni mwa vijana wenye macho lakini hawaoni na kazi yao ni kulalamika tu kama walivyolalamika wana wa Izraeli?

2.Kijana anaetaka kupata maendeleo au kutoboa kimaisha.

    • Kijana lazima aunge mkono maagizo yatolewayo na serikali yake kuhusu suala la maendeleo, kwa kufanya kazi , kujituma, kujiwekea malengo na kuwa na mipango . Lakini kama kijana atashindwa kufanya vitu hivi. Maendeleo kwake asahau,  na ajue kuwa kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa, na kupanga ni kuchagua.
    • Maisha yako uliyonayo sasa ndio uliyoyachagua kuyaishi.
  • Waliofanikiwa wote hawakuzaliwa na mafanikio lakini mafanikio wameyapata hapa hapa na si kwamba wazazi wao waliwatengenezea maisha  au waliwapa mitaji. Ila ni juhudi zao kwasababu kuna vijana wamesomeshwa na wazazi wao lakini wapo kama hawajasoma na wala hawajasaidiwa na wazazi na nafasi wanayo ya kutoka kimaisha lakini hawajishughulishi kwa lolote.

Thursday, February 13, 2020

VIJANA WALIO KOSA AJIRA NA WAMESOMA

Vijana walio kosa ajira na wamesoma tatizo lao ni kushindwa kufikirisha akili zao.
Na wasije wakafikiria kuwa na elimu ndio mwisho wa maisha bali elimu ni nyenzo rahisisho ambayo inaweza ikakusaidia kujitofautisha wewe na mtu ambaye hajasoma,
Hata kama wote mnauza genge lakini genge la msomi lazima liwe tofauti.

Sunday, January 12, 2020

VIJANA PESA NA NDOA

Ndoa za vijana nyingi zinakufa kwa kuamini kuwa mapenzi ni pesa
wasichana wengi wana aminikuwa akiolewa na mtu mwenye pesa atapata amani maishani
wavulana nao wanaamini kuwa akitumia pesa kumpata binti mrembo na akamuowa atakuwa na furaha maishani ila mimi siamini hilo naamini upendo ukitawala ndiyo kilakitu.

Je mwenzangu lipi ni sahihi kati ya hayo?

VIJANA WASOMI WENYE VYETI

Vijana wengi wakitanzania wana mawazo mgando, kwakuamini kua CV na vyeti ndivyo ambavyo vitamsababisha akapata kazi au kua na maisha mazuri lakini mimi siamini hilo, naamini kuwa utendaji wako wa kazi ndio utakufanya uweze kufanikiwa.

Je kijana wewe unaona kipi kitamsaidia kati ya vyeti na utendaji wa kazi ?

PESA NA KIJANA

Vijana wengi wanafikiri pesa ndo msingi wa maendeleo lakini mimi naamini pesa sio msingi wa maendeleo bali pesa ni matokeo baada ya mtu kufanya kazi.

JE KIJANA UNADHANI KIPI KIPO SAHIHI KWA MTAZAMO WAKO???

MALALAMIKO YA VIJANA YASIYOKUA NA TIJA

Vijana wengi wanalalamika kua serikali haijawafanyia kitu au wazazi wao hawawasaidii bila wao kujiuliza kuawameifanyia nini serikali yao au wamewafanyia nini wazazi wao.

 Mfano;

1. Serikali imewaambia vijana wajiunde vikundi vidogovidogo vya uzalishaj mali ili wapate mkopo, vijana hao hao hawataki kujiunda vikundi ila Pesa wanazitaka.

2. Utamkuta kijana mzazi wake ni mfugaji  lakini mtoto wake hataki kumsaidia mzazi wake kufuga kisasa, mzazi wake anafikia hatua ya kumuajiri mtu wakat mtoto wake yupo.

VIJANA NA MITAJI YA BIASHARA

Vijana wengi wanasema hawana mitaji ya kufanyia biashara lakini cha ajabu ukiwauliza vijana hao kua una plani yoyote ya biashara au mradi atakujibu mpaka nipate pesa,
 swali kwa vijana.
  Pesa na Mpango wa biashara kipi kinatangulia?

Monday, January 6, 2020

VIJANA KWA MWAKA 2020

NAWATAKA VIJANA WA KITANZANI WANAOTAKA  KUTOKA KIMAISHA WAFANYE MAMBO YAFUATAYO;

1. UJIFUNZE KUTOKANA NA MAMBO YOTE YALIYOKUKWAMISHA MWAKA JANA NA UYAACHE

2. KUMBUKA KUWAPUNGUZA MARAFIKI AMBAO HAWAKUKUSHIRIKISHA MAMBO YA MAENDELEO NA UONGEZE MARAFIKI WENYE MITIZAMO CHANYA

3. PANGA MIPANGO NA MARENGO YANAYO TEKELEZEKA MIPANGO YAKO IGAWANYE KATIKA MAFUNGU 3 MIPAGO YA MDA MFUPI,KATI NA MREFU.

4. KUMBUKA PESA SIO KILA KITU,KUMBUKA UWAMINIFU NI ZAIDI YA PESA.

5. KUMBUKA MTU YOYOTE ALIYE FANIKIWA ANAYO SIRI YA MAFANIKIO YAKE WALA USILILIE WALA USITAKE UTAJIRI WA MWENZAKO.

6. KUMBUKA MAISHA HAYO ULIYO SASA NI WEWE UMEYACHAGUA HAKUNA MTU ALIYE ZALIWA KUWA MASIKINI UKIAMUA UNATOKA KIMAISHA.

UMASIKINI BYE BYE KWA VIJANA

Uwanja wa vijana unawakaribisha watu mbalimbali wanaotaka kushirikiana nasi katika kuzalisha mfano kuzalishiwa kwa faida ya kila siku, wiki, mwezi hata mtu ukitaka kusimamiwa mradi wako;kubunia mradi nk. Na wakati huohuo ukiendelea na kazi zako.

VIWANDA MASHIRIKA SACOS.

UWANJA WA VIJANA UMEGUNDUA SABABU MBALMBALI ZILIZO SABABISHA VIWANDA MBALIMBALI KUFILISIKA?

BIASHARA BILA MTAJI

JE KIJANA UNAZIJUA BIASHARA UNAZOWEZA KUZIFANYA BILA MTAJI?

JE UNAJUA MUELEKEO WA VIJANA WA KITANZANIA WASIPOFANYA MABADILIKO YA KIFIKRA NA MTIZAMO NA MISIMAMO YAO?

JE WAZIJUA KAZI AMBAZO WAFANYAZO VIJANA AMBAZO NI HATARI KWA UCHUMI WA NCHI?

VIJANA JINSIA ZOTE

JE UNATAKA KUJUA MAMBO YANAYOWEZA KUKUFELISHA KATIKA MAISHA YAKO NA KUJUTA AU UPO KWENYE MAJUTO MAKUBWA AU YAKAKUSABABISHA USIFIKE KWENYE MALENGO YAKO AU NDOTO YAKO PAMOJA NA MUELEKEO WA MAISHA?