Uwanja wa vijana unashughurika na kutengeneza ajira ,kununua na,kuuza ajira,mawazo
ya biashara au miradi pamoja na kuwawezesha vijana na watu wengine kiuchumi,tunawatoa
watu kimaisha kwa pale anapo taka kufika na kuzitafuta fursa,na kuandaa mitego
mbalimbali ya kuzinasa fursa mikoa yote ya Tanzania,pia tunawasaidia wanavyuo
jinsi ya kutumia fedha wanazo zipata, pia tunatoa elimu ya fedha na matumizi ya mda,pamoja
na kuwasaidia watu wote wanao karibia kustaafu kazi ili waweze kuishi maisha
mazuri yasiyo na mapresha yanayoweza kusababisha umauti kabla ya wakati
Uwanja wa vijana umepata ufumbuzi wa mkwamo na changamoto zote walizonazo au wanazokabiliana
nazo vijana wa kitanzania baadhi ya matatizo (changamoto hizo ni pamoja na
maswala ya kiuchumi, umaskini, Ajira,mahusiano na ndoa pia uwanja wa vijana utafanya kazi ya
kuwafungua vijana vifungo mbalimbali walivyo jifunga wenyewe au kufungwa na viongozi wa dini\siasa;wazazi/vyeti vyao/mitandao/mali
za wazazi/uzuri wao/dini zao/mitizamo na misimamo yao/mila na desturi zao
nk. Uwanja wa vijana utahakikisha swala la uadui uliopo kati ya vijana na wazee unaondoka
huo wa kwamba wazee hawawezi kuwaachia nafasi za kazi kwakuwa vijana
hawajatulia na vijana wanasema wazee
wamepitwa na wakati na pia hawajasoma, pamoja na swala la kuilaumu
serikali yao kuwa haiwasaidii au ndugu na jamaa zao bila
kujua kuwa chanzo cha matatizo hayo ni wao wenyewe vijana, Uwanja wa vijana pia utafanya kazi ya
kufufua uchumi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja.ngazi ya
familia, ukoo, kijiji, kata, wilaya, mkoa hadi taifa.
Habari yako Mbokigwe
ReplyDeleteHabari nzuri ila samahani nilikuwa busy
Delete