- Unazitambua fursa zinazo tolewa na serikali kwa vijana?
- Umejiandaaje na fursa zinazoandaliwa na serikali kwa vijana?
- Je unaziona hizo fursa? Au hauna jicho la tatu la kuziona fursa hizo?
Au wewe ni miongoni mwa vijana wenye macho lakini hawaoni na kazi yao ni kulalamika tu kama walivyolalamika wana wa Izraeli?
2.Kijana anaetaka kupata maendeleo au kutoboa kimaisha.
- Kijana lazima aunge mkono maagizo yatolewayo na serikali yake kuhusu suala la maendeleo, kwa kufanya kazi , kujituma, kujiwekea malengo na kuwa na mipango . Lakini kama kijana atashindwa kufanya vitu hivi. Maendeleo kwake asahau, na ajue kuwa kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa, na kupanga ni kuchagua.
- Maisha yako uliyonayo sasa ndio uliyoyachagua kuyaishi.
- Waliofanikiwa wote hawakuzaliwa na mafanikio lakini mafanikio wameyapata hapa hapa na si kwamba wazazi wao waliwatengenezea maisha au waliwapa mitaji. Ila ni juhudi zao kwasababu kuna vijana wamesomeshwa na wazazi wao lakini wapo kama hawajasoma na wala hawajasaidiwa na wazazi na nafasi wanayo ya kutoka kimaisha lakini hawajishughulishi kwa lolote.
No comments:
Post a Comment