Sunday, January 12, 2020

VIJANA PESA NA NDOA

Ndoa za vijana nyingi zinakufa kwa kuamini kuwa mapenzi ni pesa
wasichana wengi wana aminikuwa akiolewa na mtu mwenye pesa atapata amani maishani
wavulana nao wanaamini kuwa akitumia pesa kumpata binti mrembo na akamuowa atakuwa na furaha maishani ila mimi siamini hilo naamini upendo ukitawala ndiyo kilakitu.

Je mwenzangu lipi ni sahihi kati ya hayo?

VIJANA WASOMI WENYE VYETI

Vijana wengi wakitanzania wana mawazo mgando, kwakuamini kua CV na vyeti ndivyo ambavyo vitamsababisha akapata kazi au kua na maisha mazuri lakini mimi siamini hilo, naamini kuwa utendaji wako wa kazi ndio utakufanya uweze kufanikiwa.

Je kijana wewe unaona kipi kitamsaidia kati ya vyeti na utendaji wa kazi ?

PESA NA KIJANA

Vijana wengi wanafikiri pesa ndo msingi wa maendeleo lakini mimi naamini pesa sio msingi wa maendeleo bali pesa ni matokeo baada ya mtu kufanya kazi.

JE KIJANA UNADHANI KIPI KIPO SAHIHI KWA MTAZAMO WAKO???

MALALAMIKO YA VIJANA YASIYOKUA NA TIJA

Vijana wengi wanalalamika kua serikali haijawafanyia kitu au wazazi wao hawawasaidii bila wao kujiuliza kuawameifanyia nini serikali yao au wamewafanyia nini wazazi wao.

 Mfano;

1. Serikali imewaambia vijana wajiunde vikundi vidogovidogo vya uzalishaj mali ili wapate mkopo, vijana hao hao hawataki kujiunda vikundi ila Pesa wanazitaka.

2. Utamkuta kijana mzazi wake ni mfugaji  lakini mtoto wake hataki kumsaidia mzazi wake kufuga kisasa, mzazi wake anafikia hatua ya kumuajiri mtu wakat mtoto wake yupo.

VIJANA NA MITAJI YA BIASHARA

Vijana wengi wanasema hawana mitaji ya kufanyia biashara lakini cha ajabu ukiwauliza vijana hao kua una plani yoyote ya biashara au mradi atakujibu mpaka nipate pesa,
 swali kwa vijana.
  Pesa na Mpango wa biashara kipi kinatangulia?

Monday, January 6, 2020

VIJANA KWA MWAKA 2020

NAWATAKA VIJANA WA KITANZANI WANAOTAKA  KUTOKA KIMAISHA WAFANYE MAMBO YAFUATAYO;

1. UJIFUNZE KUTOKANA NA MAMBO YOTE YALIYOKUKWAMISHA MWAKA JANA NA UYAACHE

2. KUMBUKA KUWAPUNGUZA MARAFIKI AMBAO HAWAKUKUSHIRIKISHA MAMBO YA MAENDELEO NA UONGEZE MARAFIKI WENYE MITIZAMO CHANYA

3. PANGA MIPANGO NA MARENGO YANAYO TEKELEZEKA MIPANGO YAKO IGAWANYE KATIKA MAFUNGU 3 MIPAGO YA MDA MFUPI,KATI NA MREFU.

4. KUMBUKA PESA SIO KILA KITU,KUMBUKA UWAMINIFU NI ZAIDI YA PESA.

5. KUMBUKA MTU YOYOTE ALIYE FANIKIWA ANAYO SIRI YA MAFANIKIO YAKE WALA USILILIE WALA USITAKE UTAJIRI WA MWENZAKO.

6. KUMBUKA MAISHA HAYO ULIYO SASA NI WEWE UMEYACHAGUA HAKUNA MTU ALIYE ZALIWA KUWA MASIKINI UKIAMUA UNATOKA KIMAISHA.

UMASIKINI BYE BYE KWA VIJANA

Uwanja wa vijana unawakaribisha watu mbalimbali wanaotaka kushirikiana nasi katika kuzalisha mfano kuzalishiwa kwa faida ya kila siku, wiki, mwezi hata mtu ukitaka kusimamiwa mradi wako;kubunia mradi nk. Na wakati huohuo ukiendelea na kazi zako.

VIWANDA MASHIRIKA SACOS.

UWANJA WA VIJANA UMEGUNDUA SABABU MBALMBALI ZILIZO SABABISHA VIWANDA MBALIMBALI KUFILISIKA?

BIASHARA BILA MTAJI

JE KIJANA UNAZIJUA BIASHARA UNAZOWEZA KUZIFANYA BILA MTAJI?

JE UNAJUA MUELEKEO WA VIJANA WA KITANZANIA WASIPOFANYA MABADILIKO YA KIFIKRA NA MTIZAMO NA MISIMAMO YAO?

JE WAZIJUA KAZI AMBAZO WAFANYAZO VIJANA AMBAZO NI HATARI KWA UCHUMI WA NCHI?

VIJANA JINSIA ZOTE

JE UNATAKA KUJUA MAMBO YANAYOWEZA KUKUFELISHA KATIKA MAISHA YAKO NA KUJUTA AU UPO KWENYE MAJUTO MAKUBWA AU YAKAKUSABABISHA USIFIKE KWENYE MALENGO YAKO AU NDOTO YAKO PAMOJA NA MUELEKEO WA MAISHA?